KERR ALIVYOCHUKUA POINTI TATU ZA KUKUMBUKWA ZANZIBAR LICHA YA KUTUPWA NJE YA MAPINDUZI CUP


Kocha mkuu wa Simba SC Dylan Kerr akimsogeza kijana ambaye ni mlemavu kwenye eneo ambalo angeshuhudia vizuri pambano la nusu fainali la Simba vs Mtibwa Sugar
Kocha mkuu wa Simba SC Dylan Kerr akimsogeza kijana ambaye ni mlemavu kwenye eneo ambalo angeshuhudia vizuri pambano la nusu fainali la Simba vs Mtibwa Sugar
Kocha mkuu wa kikosi cha Simba Dylan Kerr ataendelea kukumbukwa na wazanzibar wengi kutokana na kufanya kitendo cha kiungwana kwa kumsaidia mlemavu kushuhudia pambano kati ya Simba dhidi ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup.
Kerr alimchukua kijana alikua kwenye baikeli ya kiti (wheel chair) aliyekuwa amekaa sehemu ambayo asingeweza kushudia mechi hiyo kwa urahisi.  Kocha huyo wa Msimbazi alikwenda na kumtoa kutoka eneo alilokuwa amekaa na kumpeleka mbele kabisa kwenye eneo ambalo lilimrahisishia kijana huyo kushuhudia mbambano bila chembe ya chenga.
Kerr 3
Kitendo hicho kiliwafurahisha mashabiki wengi wa soka walioshuhudia kocha huyo akifanya uungwana uliotukaka na baadhi yao kumshangilia kwa kumpigia makofi.
Kerr amemfikisha kijana kwenye eneo ambalo alipata fursa ya kushudia vizuri pambano la Simba dhidi ya Mtibwa
Kerr amemfikisha kijana kwenye eneo ambalo alipata fursa ya kushudia vizuri pambano la Simba dhidi ya Mtibwa. Hapa akimkabidhi kwa huyu jamaa ambaye amevaa jezi ya njano 
Mechi ya Simba vs Mtibwa Sugar ilimalizika kwa Mtibwa kushinda kwa bao bao 1-0 dhidi ya Simba hivyo wakongwe hao wa soka la Tanzania kutupwa nje ya michuano hiyo lakini tukio la kocha huyo ndiyo lilikua gumzo uwanjani na lilibaki vichwani mwa mashabingi wa soka wa visiwani Zanzibar na litaendelea kukumbukwa siku zote kutokana na uungwana aliounesha mwalimu huyo wa soka kutoka England.




Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: