Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Miss Tanzania, Juma Pinto
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini
Dar-es-Salaam juu ya kujitoa kwao kama kamati ya kuratibu Miss Tanzania
ambayo ilichagulia na kampuni ya Lino International Agency, kushoto ni
Msemaji wa kamati hiyo Joketi Mwegelo na kulia ni Mjumbe wa kamati
Gladys Shao.
Msemaji wa Kamati ya Kuratibu Miss Tanzania Joketi Mwegelo
akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna Kamati
hiyo ilivyokuwa ikijitahidi kubadili mfumo ili kubadilisha muonekano wa
mashindano ya urembo (Miss Tanzania) kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo
Juma Pinto.
Waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa
Kamati ya kuratibu mashindano ya Miss Tanzania, Juma Pinto (hayupo
pichani) alipokuwa akitoa sababu za kujitoa kwa kamati katika mashindano
hayo. (Picha na Beatrice Lyimo-Maelezo).
Lilian Lundo- Maelezo
Kamati ya kuratibu Miss Tanzania imejitoa rasmi kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia leo tarehe 21/01/2016.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Juma Pinto alisema hayo leo, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam.
“Tumekuja kutoa taarifa kwamba, kama tulivyo teuliwa na kampuni
ya Lino International Agency, kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano
ya Miss Tanzania, kamati yangu imeamua kujitoa kutokana na majukumu ya
kamati kuingiliwa na kampuni ya Lino,” alisema Pinto.
Pinto aliongeza kwa kusema kuwa kamati yake ilipewa jukumu la
kuendesha mashindano na kuwajibika kufanya kila kitu na Lino itakuwa
kama washauri, lakini badala yake Lino imetaka kuhodhi majukumu yote na
kamati ikawa ni ya kutafuta wadhamini.
Kamati hiyo imefanya vikao vingi vya kuhakikisha mashindano
yanaboreshwa na kubadilisha mfumo ili kuifanya Miss Tanzania kuwa na
mwonekano tofauti kama ambavyo Lino ilivyoamua kuweka kamati mpya ili
kuboresha mashindano hayo.
Kutokana na kutopata muafaka katika vikao hivyo vya kuboresha
mashindano ya Miss Tanzania, Kamati ya kuratibu mashindano hayo kwa nia
njema na wala si kwa ubaya imeamua kujitoa katika Mashindano hayo.
Aidha, Pinto amewaomba radhi wadhamini ambao wameshaongea nao
kama kamati na walioonesha nia ya kuwasaidia, amewataka kuendelea
kufanya mawasiliano na kampuni ya Lino kwani madhumuni ni kudhamini
mashindano na sio kamati.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment