Wakongwe wa Nigeria na soka la Afrika kwa ujumla wakiongozwa na nahodha wa zamani wa Super Eagles Austin ‘Jay-Jay’ Okocha, Emmanuel Amuneke na Daniel Amokachi leo watakuwepo kwenye usiku wa tuzo za Glo-CAF Awards gala kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano Abuja, Nigeria.
Okocha ambaye amewahi kuzitumikia klabu za Einthract Frankfurt FC ya Germany, Fernabache ya Uturuki, Paris St Germain ya Ufaransa na Bolton Wanderers ya England anatambulika kwa aina yake ya ku-dribble mpira uwanjani. Mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya BBC alitajwa kuwania tuzo ya wakongwe (Legends Award) mwaka 2011 pamoja na mchezaji wa kimataifa wa Morocco Mustapha Hadji.
Amokachi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Everton, Club Brugges na Besiktas FC lakini pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa the Super Eagles ni star mwingine ambaye uwepo wake unatarajiwa kwenye sherehe hizo.
Lakini pia Amuneke anatarajia kuwepo, nyota huyo alicheza kama winger wa kushoto wa the Super Eagles. Hivi karibuni alikiongoza kikosi cha Golden Eaglets kutwaa taji la kombe la dunia kwa vijana wa chini ya miaka 17 (FIFA U-17 World Cup) kwenye michuano iliyofanyika Chile. Aliiwakilisha Nigeria kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 1994 huku akiwa amewahi kutamba kwenye vilabu vya Zamalek FC, Sporting Lisbon pamoja na FC Barcelona.
Wengine ni beki wa zamani wa Super Eagles Celestine Babayaro, kakayake Emmanuel Babayaro pamoja na winger wa zamani wa Super Eagles Folorunsho Okenla. Mwanasoka bora wa zamani wa Afrika Nwankwo Kanu na Victor Nosa Nosa Ikpeba pia wanataraiwa kuhudhuria kwenye tuzo hizo.
Wachezaji hao wa zamani wa kimataifa watakutana na watapata fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na wachezaji wa sasa na wazamani kutoka pembe mbalimbali za Afrika.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment