Maamuzi ya FA baada ya Jose Mourinho kukutwa na hatia ya kosa la utovu wa nidhamu


Hakika huu hauwezi kuwa msimu mbaya tu kwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho bali ni mwaka mbaya kwake, Jose Mourinho ambaye kikosi chake huwa akifanyi vizuri kwa mechi za hivi karibuni amekuwa akiingia katika headlines kutokana na kutofautiana na watu wanaomzunguuka kama waamuzi na daktari wa timu Eva Carneiro.
Usiku wa November 2 mtandao maarufu wa habari Uingereza express.co.uk uliandika maamuzi ya shirikisho la soka Uingereza FA baada ya kupatikana na hatia ya kosa la utovu wa nidhamu kwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, kocha huyo amefungiwa mechi moja na FA na kutozwa faini ya pound 40,000 kwa kosa la utovu wa nidhamu alilolionesha katika mechi aliyopoteza dhidi ya West Ham United.
Jose-Mourinho-380703
Kocha huyo wa Chelsea amekubali adhabu hiyo kutoka FA na atakosa mchezo dhidi ya Stoke City ugenini kutokana na kosa la kuwatolea maneno mabovu waamuzi wa mchezo dhidi ya West Ham United October 24 2015 tukio ambalo lilimfanya aondolewe na muamuzi katika benchi. Hata hivyo Chelsea wamepoteza jumla ya mechi sita katika mechi zao 11 walizocheza katika Ligi Kuu msimu huu. Mourinho alitenda kosa hilo wakati wa mapumziko ya mchezo huo.




Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: