Lionel Messi amekubali kujiunga na klabu ya Arsenal ila kwa sharti hili …
Staa wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi November 16 ameingia katika headlines baada ya stori zake za kutaka kujiunga na Arsenal kuandikwa katika headlines za magazeti ya Ulaya, awali Lionel Messi ambaye ameichezea FC Barcelona toka akiwa mdogo aliwahi kukiri kuvutiwa kujiunga na klabu ya Arsenal yaUingereza.
Messi ambaye wengi wamewahi kumkejeli na kudhani kuwa hana uwezo wa kutamba nje ya FC Barcelona anatajwa kuwa radhi kujiunga na Arsenal ila sharti lake la mshahara ndio tatizo linalotajwa kuwa huenda hana lengo la kwenda Arsenal, Messi anatajwa kuiomba Arsenal iwe inamlipa mshahara wa pound 600000/= kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1 za Tanzania mshahara ambao ni mgumu kwa Arsenal kumlipa hususani kwa hulka za kocha wa timu hiyo.
Stori za Lionel Messi kuvutiwa kujiunga na Arsenal aliwahi kukiri kupenda kuichezea klabu hiyo ila November 16 habari zinazotajwa kuwa za kichunguzi kutoka katika gazeti laStar Sport zinasema Messi ameombwa kulipwa mshahara kiasi ambacho ni kigumu kwaArsenal kukubali au kumudu kulipa, Lionel Messi kwa sasa anatajwa kulipwa mshahara usiofikia pound 300000/= kwa wiki na FC Barcelona na kwa upande wa Arsenalmchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ni Mesut Ozil pound 140000/= kwa wiki.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment