Kanisa la AICT Geita Lafanya ibada maalum kumuombea rais mteule

WACHUNGAJI na vingozi wa kanisa la African Inland  Church Tanzania   (AICT)  Mkoani Geita wamewataka wanasiasa ambao hawakubahatika kupata nafasi ya uongozi kwenye uchaguzi  Mkuu uliomalizika hivi karibuni  kushirikiana na wale wote walioshinda ili kuwatumikia watanzania ambao wanakiu ya kupata maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii .

Wito huo umetolewa na viongozi hao kwenye ibada maalum ya iliyofanyika katika kanisa hilo mjini Geita  kumshukuru Mungu na kumuombea Rais Mteule Dk.  John Pombe Magufuli kufuatia ridhaa aliyopata kutoka kwa wananchi wa Tanzania kupitia uchaguzi mkuu wa Octoba 25.

Wachungaji hao wamesema baada ya uchaguzi kumalizika kwa mafanikio sasa ni wakati wa kazi kwa  kushirikiana na kuwatumikia watanzania wote.

Baadhi ya waumini waliohudhuria kwenye ibada hiyo wamesema  wanaimani  kuwa Dk. Magufuli atatimiza ahadi zake alizozitia wakati wa kampeni ili kuinua maisha ya wananchi pamoja na kuchochea kasi ya maendeleo ya taifa .

Katika ibada hiyo  waumini wametumia fursa hiyo kufanya harambee kuchangia kiasi cha Milioni sita na laki tano kwa ajili ya kununua gari la kanisa hilo.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: