SECONDARY SCHOOL sehemu ya 12



SECONDARY SCHOOL

Sehemu Ya 12

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana →↓↓


"afu we pumbavu staki mazoea shuka kwenye gari chapu"
Nilishangas mtoto akianza kutoa sauti lainiiii ile dauti ya chumbani kabisaaaa ile lainiiiiiii

"shebiiii mtoto wa kiume!!! unaonekana mtoto umejaaliwa.. afu unanifukuza kwenye gari yako kweli?? sawa haina shida ila kaa ukijua sheby I LOVE YOU..... nakupenda sana sheby, na nipo tayari kukupa mwili wangu muda wowote uutakao. sheby? njoo basi unilipe chupi yangu"

SONGA NAYOOOOO



Nilianza kutetemeka mtoto wa kiume huku mtoto akianza kunisogerea na kufunua kifua chake.
"mh mh sikia kama ni hio chupi yako twende dukani ukachukue hata box zima kuliko nifanye dhambi ya ufala kama huu"
"wala sina shida ya hilo box lako kwani chupi yenyewe ni ya elfu mbili tu hivyo lengo ni kukupata wewe tu"
"sitaki sasa"
"sheby mbona kama sio mtoto wa kiume vile?"
"shakira nakuomba ushuke kwenye gari haraka sana"
"sheby? ivi upo sirias kweli?"
"shukaaaaaa tena fasta"
Nilikua nimekasirika kweli na sikua nataka utani na mwanamke.
Aliposhuka niliitoa gari mbio hadi nyumbani kwetu
Nikaingia ndani kwa hasira huku nikiwapita akina zai sebuleni... walishangaaa kuona napita spidi hadi chumbani kwangu..

Ghafla mama alikuja huku wakina zai wakiwa nyuma kwa kufata mama
"nini shida mwanangu?"
"wala tu hakuna shida mamaa"
"sasa mbona umeingia kwa hasira hivyo?"
"wala tu sina tatizo"
Mara zai kadakia juu kwa juuu
"najua tu ni kwanini?"
"we nawe tulia.. ushaanza kumchokoza kaka ako"
"mmhh sasa asiambiwe?"
"kimyaaa"
"tatizo unamdekezaaa"
"zai hunisikii? si nimekuambia kimya?"

Baada ya hapo waliondoka zao na kuniacha chumbani kwangu....
baada ya kama nusu saa hivi mama aliniita sebureni
"sheby?"
"naam?"
"njooo"
Nilifika mara moja coz si unajua mimi ndio kiziwanda afu ndio mtoto pekeee wa kiume katika hii familia hivyo heshma kwangu ilikua ni sehemu ya maisha yangu
"ndio mama?"
"sasa mwanangu? nakuomba uende ofisini mara moja"
"mamaa lakini huko kwenye duka lako la nguo si ungemuambia zai aende"
"ndio huko keshaenda zai ila mi nasemea kule head office"
"mmhhh lakini kule mi nitaweza kusimamia kweli? maana nakumbuka sijawahi kwenda hata siku moja ila nakumbuka ulinionyesha tu"
"sasa nani ataweza?, na vyote ni uridhi wako mwanangu..... we nenda afu mbona nilishawahi kukupeleka au sio wewe?"
"mmhh sio mimi ila sawa nitaenda kujaribu maana napajua kidogo"
"tatizo umezidi ubize mwanangu yani mpaka ofisi zako huzijui??? Afu sio kujaribu nenda kafanye kazi... maana ndio sehemu zako zote utakazo zizuia hivyo wapaswa kujua mapemaaaa"
"sawa mamiii nitaenda... ila nitaenda na baiskeli"
"hapana chukua gari yangu hio hapo nje au kachague gari yeyote kule uwani kuliko uende na baskeli"
"mamiii lakini si nimependa mwenyewe?"
"mmhhh sawa mwanangu ila nachukia kuigiza kama maskini mwanangu"
"wala tu mamiii"
"ok kuna zile karatasi utakwenda nazo ili ukazitie saini maana ilikua nifanye leo lakini ndio kama hivi hali imekua mbaya"
"sawa niandalie tu ili niondoke sasa hivi"
"ok sawa mwanangu"
Basi nilipewa hizo dokoment fulani na kuziweka katika bahasha kisha nikaitoa baiskeli yangu na kuanza kuiosha kwanza.... Mara alitokea dija
"kaka naomba nikusaidie kuosha"
"wala tu usijali kwani naiparua parua vumbi tu"
"sawa"
Nilimaliza kuiosha BMX yangu kisha nikaianza safari ya kuelekea ofisini kwetu
Nilikua natembea taratiibu tu huku nikiwa nimeshika dokoment za ofice katika bahasha. Na huko ninapoenda hakuna mfanya kazi yeyote yule anaenijua. labda meneja wetu ndio ananifahamu ila sio sana coz aliniona muda mrefu sana. na ilikua ni nje na kampuni....
Huko ninapokwenda ni HEAD OFFICE ( ofisi kuu ) Yaani hio ndio ofisi yetu kubwa kwa makampuni yaliopo tanzania. coz tuna makampuni mengi mpaka wazee wenyewe wanayasahau yalipi matawi hayo.... Coz kwa hapa tanzania tuna kampuni zisizopungua 10 za transpot.. na viwanda kama 6 hivi na sheli zisizopungua 4... na vyote hivyo oda zao zinatoka head office hivyo ofisi hio ni kubwa kuliko hivyo unavyofikiria... ni kama ulishawahi kuingia kwenye ofisi za T.R.A jinsi vitengo vilivyokua vingi humo ndani. coz ni ofisi yenye roshen ( gholofa ) 3
Nilikua ndio nakaribia ofisini hapo kwa kuendesha baiskeli aina ya BMX

Nilifika ofisini hapo nikakuta wafanyakazi wakiendelea kuchakalika na kazi. Afu kulikua kuna watoto duuuuuuuu kweli dingi aliajili mademu tu ila sio wafanya kazi. maana naona mademu tu ndio wanapishana...... Afu cha kushangaza askari wa geti ni demu kavaa gwanda tu..
"we mtoto unaenda wapi uko?"
"shkamoo afande?"
Niliogopa kwa kusikia hilo lisauti la kike afu linene hilo duuu... Sasa nikaona ngoja nijifanye nimekuja kuaply ( kuomba kazi) kazi
"sema shida yako kwanza"
"afande? mimi juzi nilikuja kutafta kazi sasa boss aliniambia leo nije na vyeti na CV zangu"
"we mtoto muongo sana wewe ulikuja lini hapa?"
"nilikuja juz ijumaa ila alionifungulia alikua sio wewe"
"heeee mi mbona mchana nipo kila siku?"
"mmmh labda siku hio ulienda chooni"
"pumbavu wewe unanituka mimi?"
"nisamee afande"
"nikusamee nini? toka nje?"
"jamani afande plz nina shida na kazi coz mama yangu anaumwa na baba yangu kasingiziwa kesi na kaka yangu amekufa juzi na dada yangu anajiuza tu na kuvuta bangi hivyo mimi ndio tegemezi la familia afande.. plz niruusu tu mamiii wangu"
Afande akaangalia huko na huko afu akanyoosha mkono na huku kwangu huku akisema kwa utaratiiibu
"we dogo una shing ngapi apo?"
Mmhhh nilishangaa kuona geti lenyewe linalipiwa kwa yule mtu mwenye shida ya private...
Sasa nikitaka kutoa pesa walet yangu ilikua imevimba pesa tupu hivyo akiiona hio walet ataona kua namuinjoi kutafuta kazi... labda huenda mimi ni mtu fulani ndani ya kampuni hiii...
"kwani unataka shing ngapi afande?"
"kaki tu inatosha dogo..fanya fasta"
"sasa afande? utanidai bac nikitoka coz hapa nina efu kumi tu"
"dogo unanizoea?"
"basi afande nakupa mama"
Nilijisachi sana ilimladi tu nisiitoe walet, maana walet yangu ilikua hata kubana haibani ng'ooo kwa wingi wa pesa.... Nilibahatisha elfu kumi kwenye mfuko wa shati hivyo nikampa ile elfu kumi..
"nipe basi chenchi afande?"
"chenchi ya nini?? hebu nenda uko"
"afande sijala eti mchana"
"sasa inaniusu mimi? au nikutoe nini?"
"aaah ah basi chukua tu"
Nilipita vizuri getini japo ni kwa mbinde...

Nilipita moja kwa moja hadi kwa secretary wa kampuni hii. aisee ni mzuri huyo duuu
"za saa iz dada?"
Yaani kwanza aliniangalia kuanzia chini mpaka juuu. coz nilikua nimevaa kawaida tu wala sijavaa suti wala kulipuka... bali nilivaa mbano wangu na tishet kali afu nikatingishia na kibarakashee kwa juu..
"salama nikuseidie nini?!
"naomba nimuone meneja muajiri tafadhali"
"meneja??? una apointment nae?"
"mh mh hapana sina"
"ok kaa pale nimuulize"
Nikakaa mtoto wa kiume huku nikiona visketi tu vikijipitisha tu mbele yangu
Mara kuna mtoto mkali katoka kwenye kitengo chake na kunifata mimi
"mambo?"
"safi tu shkamoo?"
"heee unamuamkia nani sasa?"
"si wewe"
"weeeeeee mi bado mschana wewe"
"sasa mbona umejifunga manguo hadi usoni?"
Nilimzingua but hivyo ndivyo ninavyotaka mimi. watu wavae kiheshima
"weee ofisini kwetu hua tumeambiwa tukivaa kimini unafkuzwa kazi"
"kwaio kumbe umevaa kwa ajili ya kazi tu?"
"ndio"
"mmhhh haya"
"vp umeleta oda nini?"
"kwani vp?"
"ah ah naona umeshika madocoment apo"
"wala tu nimekuja kuomba kazi"
"koho koho ukoho ukoho koho oooohhh duuu umesemaje vile?"
"nimekuja kuomba kazi humu kwenu"
Akamgeukua secretary na kumuambia kua
"sesi? unamsikia uyu mtoto?"
"kanasemaje ako?"
"eti kamekuja kuomba kazi?"
"heeeeeee hako kataweza kazi za humu kweli hako katoto"
"nashangaaa.... afu we dogo humu kwenye kampuni hii hawaajiri watoto wadogo kama wewe"
"lakini nina miaka 20 jamani"
"heeeeee kumbe bado toto"
Mara secretary akasema kua
"we dogo? umeishia langapi?"
"mhhh darasa la saba"
"puuuuhahahahahahahahaha sasa lasaba nani atakuajiri?"
"jamini lakini hapa nina CV na cheti cha kumaliza darasa la saba"
"we unatupotezea tu muda hapa.. we nenda kaendelee kusoma uko"
Sasa sijakaa vizuri mara wakatoka wafanyakazi wote. maana ilikua ni muda wa kwenda kula lanchi
"heee we sesi haka katoto ni ka nani?"
Sasa wale waliokua wakitoka ndioa wakawa wanasemezana
"afu ni kahensamu"
"we dogo mambo?"
"poa shkamoo?"
"heeeeee anamuamkia nani sasa?"
"mwenzangu hata mi nashangaa"
"kana heshma eee?"
"sanaaa"
Mara meneja katoka huku kakunja sura hio duuu
"sesiiiiii?"
"ndio boss?"
"ulisema kuna mgeni wangu?"
"ndio ni huyo hapo"
"huyu mtoto huyu ndio ananiita kwa mkwara wote huo?"
"ndio afu anataka kazi"
Nikadakia juu kwa juuu huku nikisimama
"ndio nataka kazi bosi"
"tulia wewe funga domo lako ilooo"
Nilikaaaa kwa unyongeee huku nikiwasikilizia
Mara kuna wengine wanne wamekuja kuomba kazi wako na mavyeti yao....
Walianza kumsalimia meneja huku wakiinama ile kiheshima.
"shkamooo boss?"
"marahaba hamjambo?"
"hatujambo boss?"
"Enhee shida ni nini?"
"boss tumekuja kuomba kazi"
"ivi nyie hapo nje kuna bango limeandikwa kua hapa kuna kazi?"
"hapana boss ila tumekuja tu kwakua tulisikia kua kuna nafasi"
Nilijikuta nimedakia juu kwa juu
"eti bosi kumbe kuna nafasi za kazi?? nipe basi bosi"
"we mtoto acha mdomo mchafu..... afandeeee? afandee? we afande?"
"abee bosi?"
"toa hizi taka taka hapa?"
"sawa afande"
Daaahh tulianza kushikwa tanganyika jeki na yule afande wa kike
"afande utatuumiza bwana"
"tokeniiiii"
Nikaona hapana hii sio haki kabisa
"afande niachie haraka"
"unasemaje we mtoto?"

Usikose kesho

Press LIKE kuisapot ihepeeeee

Ani ni #YediDay

via~ #TeamDwacBoy


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: