Octoba 15, 2015 taarifa ya Majonzi
ilitufikia ambapo taarifa yenyewe ilikuwa inahusu msiba wa watu wanne
wakiwemo Mbunge wa Ludewa Deo Haule Filikunjombe na aliyekuwa Baba mzazi
wa meya wa Ilala, William Silaa baada ya kupata ajali kwenye helikopta
iliyoanguka katika msitu wa mbuga ya Wanyama ya Selous.
Taarifa kuhusu Ratiba ya kuwasili kwa
miili hiyo Dar es Salaam na shughuli za kuaga miili hiyo pamoja na
Ratiba ya Mazishi tayari ilitolewa, ambapo leo Octoba 17, 2015 marehemu
Deo Haule Filikunjombe pamoja na wengineo waliofariki kwenye ajali hiyo
ya helikopta waliagwa Mbagala Dar es Salaam kuelekea Ludewa mkoani
Njombe kwaajili ya mazishi.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment