Mgombea wa urais katika shirikisho
la soka duniani Fifa mwana mfalme Ali Bin al-Hussein anasema kuwa
kucheleweshwa kokote kwa uchaguzi wa kumteua mrithi wa Sepp Blatter
kutaliyumbisha shirikisho hilo zaidi.
Raia huyo wa Jordan anataka kumrithi Blatter aliyesimamishwa kwa mda katika uchaguzi wa mwezi Februari.Lakini Blatter mwenye umri wa miaka 79 pamoja na rais wa UEFA Michel Platini walisimamishwa kazi kwa mda huku FIFA ikitarajiwa kujadiliana kuhusu kuahirisha uchaguzi huo.
Ali amesema kuwa hatua hiyo itatoa funzo kote duniani,
Blatter na Platini wote wameenda mahakamani kupinga kusimaishwa kwazi kwa siku 90.
Katibu mkuu Jerome Valcke pia amesimamishwa kazi.Wote watatu wamekana kufanya uovu.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment