Mabingwa
wa mbio za wanawake katika Tamasha la Majimaji Selebuka. Kutoka kulia
ni bingwa wa mbio za kilometa tano za wanawake, Neema Ndambo,
Mwanaharabu Pili aliyeshika nafasi ya pili na mshindi wa tatu, Shakira
Abdallah.
Mama
na mwana….Bibie Abdallah kushoto akiwa katika pozi na mwanaye, Shakira
Abdallah, wote walishiriki katika mbio za wanawake za Km 5, katika
Tamasha la Majimaji Selebuka. Mama ameshika nafasi ya tano, mwana nafasi
ya tatu.
Washindi wa mbio za wanawake katika picha ya pamoja na viongozi wa tamasha la Majimaji Selebuka 2015.
Washiriki wa mbio fupi za wanawake wakiwa wamepumzika baada ya kukimbia.
Shakira
Abdallah akimalizia mbio katika shindano la mbio za wanawake Km 5
zilizoandaliwa na Asasi ya Somi katika Tamasha la Majimaji Selebuka
2015. Shakira ameshika nafasi ya tatu licha ya kukimbia peku.
Mkurugenzi
mwenza wa Asasi ya Songea-Mississippi, Dk Damas Ndumbaro kulia akipata
maelezo kutoka kwa wajasiriamali katika maonyesho ya wajasiriamali
kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2015, kwenye Uwanja wa Makumbusho ya
Mashujaa wa Vita vya Majimaji, mjini Songea.
Mmoja
wa askari barabarani akiwa na cheti alichotunukiwa katika Tamasha la
Majimaji Selebuka 2015 linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya
Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.
Bingwa
wa mbio za wanawake, Neema Ndambo akishangilia baada ya kuvishwa medali
ya dhahabu na kupokea kitita cha fedha tasilim katika Tamasha la
Majimaji Selebuka 2015
Wananchi
mbalimbali wakipata ufafanuzi kutoka kwa wajasiriamali katika maonyesho
ya bidhaa zao kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 linaloendelea
kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.
Washindi wa mbio za wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa tamasha la majimaji selebuka.
Mkurugenzi
mwenza wa Asasi ya Songea-Mississipi, Prof. Julian Murchison akipewa
maelekezo na wajasiriamali katika maonyesho ya bidhaa zao kwenye tamasha
la majimaji selebuka 2015.
Mshindi
katika mdahalo wa Tamasha la Majimaji Selebuka Jonathan Patrick
(katikati) kutoka shule ya Kigonsera High School, mshindi wa pili ni
Mwajuma Hassan kushoto kwake wa Shule ya Sekondari ya Londoni na
Godliving Bayona wa Kigonsera aliyeshika nafasi ya tatu.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment