MATOKEA YA URAIS: DK MAGUFULI ANAONGOZA MAJIMBO 17, LOWASSA MAJIMBO 10...




Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Usiku huu imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 27 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza kwa majimbo 17 wakati Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa anaongoza majimbo 10.


Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa awamu tatu, ambapo asubuhi mwenyekiti huyo alitangaza majimbo matatu ambayo ni Paje, Makunduchi na Lulindi ambayo yote Dk Magufuli ameongoza.

Majira ya alasiri , Jaji Lubuva alitangaza majimbo mengine 10 ambapo kati ya hayo majimbo sita yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo manne yakionyesha Lowassa anaongoza.

Usiku huu majira ya saa mbili , Jaji Lubuva ametangaza majimbo mengine 14 ambapo kati ya hayo majimbo 8 yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo 6 yakionyesha Lowassa anaongoza.
Majimbo hayo ni kama ifuatavyo:
Matokeo ya Urais Singida Mjini
Kura: 56,558 
Magufuli (CCM): 36,035 
Edward Lowassa (Chadema): 19,007






Matokeo ya Urais Jimbo la Lindi Mjini 
Kura: 38,992 
Magufuli (CCM): 21,088 
Edward Lowassa(Chadema): 17,607 

Matokeo ya Urais Jimbo la Njombe Mjini 
Kura: 55,772 
Magufuli (CCM): 33,626 
Edward Lowassa(Chadema):20,368

Matokeo ya Urais Jimbo la Peramiho 
Kura:45,374 
Magufuli (CCM): 32,505 
Edward Lowassa (Chadema): 11,291

Matokeo ya Urais Jimbo la Mkinga 
Kura: 39,788 
Magufuli (CCM): 23,798 
Edward Lowassa (Chadema): 15,142

Matokeo ya Urais Jimbo la Moshi Mjini 
Kura:79,814 
Magufuli (CCM): 28,909
Edward Lowassa (Chadema): 49,379

Matokeo ya Urais Jimbo la Nanyamba 
Kura: 44,437 
Magufuli (CCM): 24,904 
Edward Lowassa (Chadema): 16,992

Matokeo ya Urais Jimbo la Mbinga Mjini 
Kura: 42,717
Magufuli (CCM): 29,295 
Edward Lowassa (Chadema):11,695

Matokeo ya Urais Jimbo la Kisarawe 
Kura: 38,012 
Magufuli (CCM): 24,086
Edward Lowassa (Chadema): 13,093

Matokeo ya Urais Jimbo la Mgogoni 
Kura: 7,539 
Magufuli(CCM):710 
Edward Lowassa (Chadema): 6,506

Matokeo ya Urais Jimbo la Mtambwe 
Kura: 7,620 
Magufuli (CCM): 428 
Edward Lowassa (Chadema): 6,937


Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo ya majimbo mengine ambayo yatakuwa tayari yatatolewa kesho saa tatu asubuhi.

 Bonyeza Picha Kuyaona Vizuri




























Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: