Mwanaume ambaye hajafahamika jina lake, amefika kwenye kituo cha kupiga kura cha Mtoni Kijichi A, kisha akaanza kuhubiri kwa sauti kubwa akimwomba Mungu awabariki wapiga kura.
Wakati akiendelea kuhubiri alikuwa akielekea kwenye chumba cha kupigia kura.
"Mungu awabariki mpige kura kwa amani, mbarikiwe, jamani mnanisikia?" Alisema.
Hata hivyo mtu huyo aliyekuwa akizungumza huku akipepesuka, alizuiwa kuingia kupiga kura na askari aliyekuwa mlangoni kwa madai kuwa hakuwa amefuata taratibu.
Baada ya askari kuzungumza nae alitaka aruhusiwe kuingia kupiga kura, lakini baadhi ya wananchi walipinga wakisema mtu Hugo ni mlevi.
"Kalewa huyo tunamjua akapange mstari kule nyuma," alisema mmoja wa wapiga kura
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment