WANANCHI LUILO WAMCHOKA DIWANI

WANANCHI wa kijiji cha Luilo kata ya Luilo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wamemkataa mbele ya mbunge Deo Filikunjobe,diwani wao wa kata ya Luilo Matei kongo (CCM) ambae ni mwenyekiti wa Halmashauri yaLudewa na kutaka acharazwa bakora hadharani kutokana na kuwa mpinzani wa maendeleokatika kata ya Luilo.Wananchi hao walimlalamikia diwani huyo katika mikutano ya hadhara wa mbunge Filikunjombe aliyoifanya kwenye vijiji vya Lifua na Luilo kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushirikiana na mkandarasi wa mradi wa umeme katika shughuli za kuchimba mashimo .Wakizungumza katika mkutano huo wananchi hao walisema kuwa wanashangazwa na hartua ya diwani wao mbali ya kuwa ni diwani wa CCM ila ameendelea kuwa mpinzani mkubwa wa maendeleo katika kata yake kwa kupinga kila shughuli ya maendeleo inayofanywa mbunge katika kata yake.mkazi wa kijiji cha Luilo Osward Haule alisema wakati serikali ya CCM ikihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za kmaendeleo kwa kujitolea nguvu zao diwani huyo amekuwa akienda kinyume kwa kuzuia wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo na kuwa katika kata hiyo kuna ujenzi wa zahanati unaoendelea kwa zaidi ya miaka minne sasa bila kukamilika kutokana na ubinafsi wa diwani huyo.' mbunge wetu umekuwa ukifanya kazi kubwa sana ya kutuletea maendeleo katika jimbo la Ludewa na hatujapatakuwa na mbunge anayejitumakuleta maendeleo kama wewe toka nchi hii ipate uhuru ila kikwazo kikubwa kipohapa
mbele kwenu viongozi kwani diwan wetu kweli tunashindwa kumuelewa na mpinzani ama ni diwani wa ccm kila jema linalofanywa nambunge yeye kazi yake ni kupinga ......sasa inapendezwa sana wapinga maendeleo wakati mwingine kuonywa kwaviboko'Alisema kuwa sababu kubwa ya kata hiyo kukwama baadhiya miradi ya kimaendeleo ni kutokana na diwani wao kuwa kibinafsi zaidi na kuonyesha wazi wazi upinzani wa kazi zinazofanmywa na mbunge hivyo kwa upande wao wanamtaka diwani huyo kukaa pembeni ili wao wateue diwani wao wa muda atakayeshirikiana na mbunge kuwaletea maendeleo kwa muda uliobaki na baada ya hapo muda wa uchaguzi ukifika wamchague diwani wa wananchi nje ya diwani huyo.kwani alisema wao kama wananchi wapo tayari kwendakushiriki maendeleo ila shidaipo kwa diwani ambae amekuwa akiwazuia kushiriki shughuli za kimaendeleo hasa katika miradi inayoanzishwa na mbunge .Hata hivyo alisema kwenye kijiji hicho kuna mradi wa ujenzi wa zahanati ambao umeendelea kukwama kwa zaidi ya miaka minne sasa huku kazi kubwa ya diwani wao ni kujitolea gari la kusafirisha maiti kutoka Halmashauri pindi wananchi wa kata hiyo wanapopatwa na msiba badla ya kusimamia ujenzi wzahanati hiyo ili kupunguza vifo.mwenyekiti wa kijiji cha kipangala Jeremia kayombo alimweleza mbunge huyo katika mkutano kuwa diwani huyo alimpigia simu siku mojabaada ya mbunge kupita kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za uchimbaji mashimo ya nguzo za umeme akimtaka azuie wananchi wasishiriki maendeleo japo viongozi na wananchi walimpuuza.'mimi kama mwenyekiti wa kipangala ninae tokana na ccmsipotayari kusema uongo hapanitasema kweli tupu kama chama chetu ccm kinavyotakahuyo diwani ni mpinzani mkubwa wa maendeleo alinipigia simu kutaka nizuie wananchi kushiriki katika maendeleo'Alisema hata sababu ya kutoshiriki katika mikutano hiyo ya mbunge kwa diwani huyo ni kutokana na kukwepa hasira za wananchi dhidi yake japo mara kwa mara mbunge anapofanya ziara katika kata yake huwa anatoa sababu mbali mbali za kutoshiriki .Akiwahutubia wananchi hao mbunge Filikunjombe mbali ya kuwapongeza kwa hatua waliyoichukua ya kumpuuza diwani huyo bado alisema kwa upande wake kama mbunge hatapenda kuona wananchi wakikosa maendeleokutokana na vikwazo vya kiongozi mmoja na kuwa kwa nguvu zake na ushirikiano wa wananchi wa kata hiyo lazima umeme ufike.Filikunjombe alisema yupo tayari kugombana na mtu mmoja anayekwamisha maendeleo na mara baada ya umeme kuwaka atapatana ila si vinginevyo kwani wanaopata shida ni wananchi na sio viongozi .Alisema kuwa ni kweli serikali imetoa pesa kwa mkandarasi kwa ajili ya umeme ila kwa kasi ya mkandarasi uwezekano wa umeme huo kukamilika mwaka huu ni ndoto kutokana na kasi ndogo na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo ni mmoja kwa mkoa mzima wa Njombe hivyo kwa upande wake kwa kutumia mbinu zake amefanikiwa kupata nguvu na kutaka umeme huo kuwaka baada ya miezi miwili kwa vijiji vyote zaidi ya 12 vya jimbo la Ludewa.Mbunge huyo alisema kuwa baadhi ya maeneo umeme umekuwa ukichelewa kufika kutokana na wananchi kuleta vikwazo vya kudai fidia ya miti na mazao ila kwa wilaya ya Ludewa amefanikiwa kuwaomba wananchi wasidai fidia ya miti na wao wenyewe kushiriki kuchimba mashimo na wamekubali katika kata zote na madiwani wanashiriki vizuri katika maendeleo ila shida ni kwa diwani huyo wa Luilo .kuwa gharama ya uchimbaji shimo moja ni Tsh 5000 na kuwa jumla ya mashimo kama 15 hivyo ni kiasi cha sh 75,000 ambazo kama kulipwa wananchi hao wangelipwa na ukigawa kwa kila mwananchi ni kama sh 150 na kama kazi hiyo ya uchimbaji ingefanywa na mkandarasi kwa mafundi wake ingechukua muda mrefu zaidi hivyo ndio sababu ya kuwaomba wananchi kujitolea nguvu zao.Pia alisema kwa upande wakekwa ajili ya kuwaunga mkono atawasaidia kukamilisha zahanati hiyo ili kuepukana nashida ya zahanatiAkizungumza kwa njia ya simu kuhusiana na malalamiko ya wananchi wakediwani Kongo alikiri kuwazuia wananchi kushiriki katika maendeleo ya mradi huo wa umeme huku akidai kuwa yeye ni mwenyekiti wa halmashauri ya Ludewa .Kongo alisema kwa kuwa mkandarasi kapatikana hata kama wananchi watapata umeme kwa kuchelewa ni sawa tu .mkandarasi wa mradi huo wa umeme Bw Aron Makulu alisema alisema kuwa kampuni yake uwezo haina uwezo wa kuwalipa wananchi pesa ila fedha zilizopo za kulipa wafanyakazi pekee.katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama kizuri sana kinachowajali wananchi wake ila shida ni baadhi ya viongozi ndio wanaokichafua chama na kuwafanya wananchi wakione chama kibaya na kuwa kama chama hakitakubali kuchukiwa na wananchi kwa ajili ya mtu mmoja na kuwataka wananchihao kuwapuuza viongozi wasiopenda maendeleo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: