Wananchi Chunya walala chini wakiomba waziri mkuu kuigawa wilaya yao Waziri mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda ameahidi kuigawa wilaya ya Chunya ili kupata wilaya mbili kabla ya uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Uamuzi wa waziri mkuu kuigawa wilaya ya Chunya haraka unatokana na maombi ya wananchi wa jimbo la Songwe hususan katika kijiji cha Buyuni ambao wameamua kulala chini kwenye mavumbi, huku mbunge wa jimbo la Songwe, Mheshimiwa Philip Mulugo akipiga magoti chini na kumwomba waziri mkuu kuigawa wilaya hiyo kwa madai kuwa ina maeneo makubwa kijiografia hali ambayo inakwamisha maendeleo ya wananchi. Mkuu wa mkoa wa Mbeya akamweleza waziri mkuu kuwa ukubwa wa wilaya ya Chunya ni asilimia 46 ya ardhi yote ya mkoa wa Mbeya hivyo maombi ya wananchi hao yana hoja ya msingi, huku wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akielezea uwezo wa halmashauri ya wialaya ya Chunya kiuchumi kuwa inajitegemea kwa asilimia 15. Waziri mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema kuwa kikwazo pekee cha kuigawa wilaya hiyo ni idadi ndogo ya watu, lakini kutokana na hali ambayo ameiona analazimika kuigawa wilaya hiyo haraka, jambo ambalo ameahidi kulifanya kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: