Ufafanuzi juu ya Hali ya Afya ya Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai

Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya kijamii kuhusu hali ya Afya ya Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Ofisi ya Bunge inapenda kuutangazia umma na Wananchi wote kuwa, taarifa hizo zinazosambazwa katika baadhi ya Mitandao si za kweli, bali ni uzushi mtupu. Ukweli ni kwamba Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ni Mzima wa afya na hivi sasa yuko jimboni kwake Kongwa, Mkoani Dodoma akifanya maandalizi ya Mwisho ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii na hasa Jimboni Kongwa, Dodoma. Ofisi ya Bunge inapenda kuwatoa hofu Wananchi wote na kuwataka kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa si za kweli bali ni uvumi unaonezwa na watu wachache wenye nia ovu ya kujenga hofu miongozni mwa Wananchi kupitia mitandao ya kijamii. Aidha tunapenda kutoa rai kwa watu wote kuacha kusambaza taarifa hizo potofu na badala yake kama kuna taarifa zozote kuhusu Ofisi ya Bunge au Viongozi wake wafanye jitihada za kuthibitisha taarifa hizo kwenye Mamlaka husika kabla za kuzisambaza. Ofisi ya Bunge inao utaratibu rasmi wa kutoa taarifa muhimu kwa wananchi na umma kwa ujumla, hivyo si vyema kwa watu kusambaza taarifa potofu kuhusu Bunge na viongozi wake ambazo zinaweza kuleta usumbufu miongoni mwa Viongozi na baadhi ya wananchi. Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge DAR ES SALAAM 4 MACHI 2015
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: