Q-Chillah,TID wataka kutwangana ngumi kisa,ngoma mpya ya Ali Kiba



Mastaa wa Bongo Fleva,Q-Chillah na TID mwishoni mwa wiki hii walitaka kutwangana walipokutana katika Klabu moja usiku.Kwa mujibu wa Q-Chillah akizungumza kwenye Uheard na Soudy Brown alisema kuwa alikwenda kwenye klabu hiyo kuangalia shoo iliyokuwa ikifanyika kwenye lakini baadaye aliamua kutoka nje kucheza ‘pool table’ ndipo alipomuona TID.
‘’Nilimuona jamaa(TID) akiniangalia na baadaye alinifuata akaniambia kuwa anataka kuongea na mimi nikamwambia ile siye sehemu yake atafute muda mwingine ndiyo tuongee,’’alisema Q-Chillah.

 Aidha Chillah aliongeza kuwa TID aliendea kumuongelesha ndipo alimwambia kuwa anachofanya kumuongelea yeye vibaya siyo vizuri na kile alichokipost hivi karibuni kuhusu kuuponda wimbo mpya wa msanii Ali Kiba uitwao ‘Cheketua’ aliouachia hivi karibuni kupitia account yake ya Instagram hakikuwa kitu cha busara ilitakiwa amsapoti kama msanii mkongwe kuliko kumponda hadharani kupitia mitandao.

 ‘’Kiukweli kitendo cha TID kuandika Instagram kuwa ngoma mpya ya Alikiba ni mbaya na baada ya miezi mitatu haitokuwepo siyo kizuri nilimwambia yeye ni msanii mkubwa inabidi kumsapoti Ali Kiba na kwamba nilitaka kumpiga kwa fimbo ya pool table siyo kweli nilikuwa nikimueleza tu,’’aliongeza Q-Chillah. 

Kwa muda mrefu wasanii hao wawili ambao waliwahi kuwa pamoja kwenye bendi ya (Top Band) wamekuwa kwenye bifu zito wakitupiana maneno kwenye vyombo vya habari.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: