KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema kama alivyotoa taarifa juzi tarehe 04/02/2015 kuhusiana na kuawa kwa Askari Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI huko Chang’ombe ya juu mkoani Dodoma na mtu aliyefahamika kwa jina la TISSI S/O SIRIL MALYA. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga kichwani na mikononi askari huyo. Kamanda MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti Mkavu Mailimbili mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua askari. Hata hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki. Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: