COASTAL Union wamegoma kufungwa mechi ya pili mfululizo nyumbani, baada ya jioni ya leo kulazimisha sare ya 0-0 na Simba SC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba ilijaribu kutengeneza mashambulizi ya mipira ya kutokea pembeni, lakini washambuliaji wake Dan Sserunkuma na Elias Maguri walibanwa na walinzi wa Coastal.
Hali kadhalika Coastal nayo ilitengeza mashambulizi yake kadhaa, lakini washambuliaji wake Iker Obinna na Rama Salim walibanwa na mabeki wa Simba SC.
Hakukuwa na mchezo wa kuvutia sana kutokana na timu zote kucheza mipira mirefu kwa kuhofia ubovu wa Uwanja wa Mkwakwani, lakini hakukuwa na kupamiana kama ilivyokuwa Jumatano Coastal ikifungwa 1-0 na Yanga SC.
Refa wa mchezo Simon Mbelwa aliyesaidiwa na Abdallah Mkomwa na Frank Kombo wote wa Pwani, kwa kiasi kikubwa walijitabhidi kuumudu mchezo huo.
Kwa matokeo hayo, Coastal inafikisha pointi 18, wakati Simba SC inatimiza pointi 17.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment