Wanamgambo wamemteka naibu waziri wa maswala ya kigeni katika serikali inayotambuliwa kimataifa nchini Libya.
Maafisa wanasema kuwa Hassan al Saghir alitekwa nyara kutoka chumba chake cha hoteli katika mji wa mashariki wa Al-Baida mapema jumapili.
Haijulikani ni kundi gani lililotekeleza kisa hicho.
Utekaji nyara umekuwa jambo la kawaida nchini Libya,ambapo serikali mbili zinapigania udhibiti huku makundi tofauti ya wanamgambo yakikabiliana.
Via>>BBC
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment