Nahodha Yassine Chikhaoui ameisaidia timu yake ya Tunisia kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Zambia.
Ushindi huo umeifanya Tunisia kuongoza Kundi B katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika inayofanyika Equatorial Guinea ikifikisha pointi nne.
Chikhaoui alifunga bao katika dakika za mwisho kwa kichwa akiunganisha krosi iliyompita kipa Kennedy Mweene na kupoteza matumaini ya Wazambia.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment