TAIFA SATARS MABORESHO, AMAVUBI ZAMALIZA KWA SARE YA 1-1 KIRUMBA

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kimefanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Rwanda maarufu kama Amavubi. Katika mechi hiyo ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Rwanda ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mzoefu Jean Baptiste Mugiraneza kwa kichwa baada ya mabeki wa Stars kufanya uzembe. Stars ilisawazisha baadaye kupitia Kelvin Friday Iddi ambaye hata hivyo hakucheza vizuri katika mechi hiyo. Kiungo Simon Msuva wa Yanga ndiye aliyekuwa msumbufu zaidi kwa mabeki wa Amavubi iliyoongozwa na Haruna Niyonzima. Mashabiki walijitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: