SHEREHE YA ‘ESCROW’ NOMA, WATOTO WA KIGOGO WAFANYA BETHIDEI YA MAMILIONI

WAKATI dunia ikiingia Mwaka Mpya wa 2015, taarifa ikufikie kwamba kigogo mmoja ambaye ni mfanyabiashara maarufu jijini Dar amewaangushia wanaye, Hassan na Khadija Dilunga sherehe ya kuzaliwa ambayo imepachikwa jina la ‘Escrow’ kufuatia kufuru ya fedha iliyooneshwa na wahusika hivyo kuwa ndiyo gumzo la mjini kwa wikiendi iliyopita. MSHANGAO! Sherehe hiyo ilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar juzi ambapo waalikwa wengi walijikuta wakibaki midomo wazi kwa vile wakati wanafika nje walijua ni harusi ya mtoto wa mtu mzito serikalini lakini walipozama ndani walipigwa butwaa kukuta ni ‘bethidei’. “Du! Ni sherehe ya aina yake, watoto wameingia kama maharusi kwa kumwagiwa maua tena wana ‘meidsi’ na upambaji wa ukumbi unatisha, naona umesheheni mapambo ya gharama kubwa,” alisikika akisema mwalikwa mmoja huku akiendelea kushangaa maandalizi hayo ya kukata na mundu kama si shoka! KULA, KUNYWA ZAIDI YA HARUSINI Taarifa zaidi zinasema kuwa, waalikwa walikula vyakula vya kila aina tena vya gharama. Walikunywa mvinyo wa bei mbaya na vitu vilikuwa vya kumwaga kuliko hata inavyokuwa harusini.” Keki za kifahari na shampeni kibao. WABADILI NGUO UKUMBINI Kama vile haitoshi, watoto hao wakiwa ukumbini hapo huku wakikata keki kubwa na kulisha wazazi na wageni waalikwa, kuna wakati walikwenda kubadilisha nguo ambapo kama mwalikwa aliwaona wakati wanaingia, ilikuwa tofauti na wakati wa kutoka. Hassan kwa juu alivaa T-shirt iliyoandikwa Air Jordan ambapo ilikuwa sare na ya baba yake aliyevaa naye Air Jordan. JEURI YA FEDHA Lilipowadia suala la kutuza sasa, watoto hao walimwagiwa mifedha hasa noti nyekundu (msimbazi) na madolari (dola) hadi wakajaza vikapu viwili walivyovishika mapajani. Hata hivyo, haikujulikana kiasi cha pesa kilichopatikana! ZAMU YA MAMA WATOTO SASA Mama huyo wa watoto hao (Tunt) naye ilipofika zamu yake ya kutoa zawadi, aliwapa simu aina ya Sumsung Galax note 3 na mikufu ya dhahabu ambayo kwa mwonekano ni kuanzia gramu tano na kuendelea. Waalikwa wakifungasha fedha ukumbini. FUKO LA FEDHA Katika hali ya kushangaza, mama huyo alijaza fedha kwenye FUKO LA RAMBO na kuondoka nalo, utadhani ilivyokuwa kwa waliochota fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo kwa sasa ni gumzo nchini kote. “Jamani naona leo hapa ni kama Escrow kwa kwenda mbele. Hebu angalia ule mfuko ya rambo, umejaa fedha. Sijui ndiyo mifuko aina ya sandalusi aliyoisema Zitto Kabwe? (mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali).
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: