Wanawake wilayani ludewa katika mkoa wa njombe wametakiwa kuwa viongozi kwa jamii katika kuelimisha jamii juu ya mchakato wa kuipigia kura katiba mpya inayopendekezwa ifikapo april 30 mwaka huu.
Akizungumza na baraza la wanawake wa chama cha mapinduzi ccm hivi karibuni wilayani ludewa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya ludewa bw, Stanley kolimba ambae pia aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la ludewa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ccm alisema kuwa katiba inayopendekezwa imebeba mambo mengi yanayoitetea jamii hasa wanawake hivyo mwanamke nilazima aielimishe jamii juu ya kufanya maamuzi bora kwa manufaa ya taifa.
Alisema kwakuwa wanawake wanaishi na kuilea jamii hasa familia zao hivyo wananafafasi kubwa sana ya kuweza kusikilizwa ili kuweza kuboresha miundombinu ya taifa la tanzania kwakuwa kwasasa kila mwananchi anamaoni tofauti juu ya mchato huo wa katiba inay6o pendekezwa.
Katika baraza hilo la wanawake alihudhuria pia aliyekuwa mjumbe wa bunge la katiba mh, Suzani kolimba ambaye alitakiwa kuwaelimisha wanawake wenzake juu ya faida na hasara zinazoweza kujitokeza wakati wa kuipigia kura katiba hiyo inayopendekezwa.
Hatahivyo mwenyekiti huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa chama hicho kushirikiana na serikali ya halmashauri ya wilaya ludewa kuhakikisha wanaandaa na kugawa kwa wananchi Rasimu ya katiba inayopendekezwa kwalengo la kuwapa wananchi ili waweze kuzipitia kwalengo la kufanya maamuzi mazuri wakati wa kuipigia kura ya ndiyo au hapana licha ya kuwa muda uliobaki ni mchache zaidi.
''Katibu wa chama nakuomba hakikishe unafuatilia kwa haraka rasimu hiyo ili uwagawie watu waweze kuzisoma kwa makini na hatimaye waweze kuipigia kura baada ya kuielewa Alisema bw. Kolimba ambaye ni mwenyekiti wa ccm wilaya ya ludewa''
Kwa upandewake katibu wa chama hicho wilaya ya ludewa bw, Elyudi Shemauya alisema kuwa atahakikisha kuwa anazipata rasimu hizo kwaajili ya kuwapa wananchi ili waweze kuipigia kura ifikapo april 30 mwaka huu.
Home
Uncategories
MWEKITI WA JIMBO LA LUDEWA MKOANI NJOMBE CCM, STANLY KOLIMBA AZUNGUMZA NA WANAWAKE WA CHAMA HICHO WILAYANI LUDEWA,
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment