Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda ameifungia timu yake bao pekee dhidi ya Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara, Mrwanda alifunga bao hilo dakika ya 42 dhidi ya timu yake ya zamani akiunganisha krosi safi kutoka kulia mwa uwanja.
Kipindi cha kwanza kilionekana kuwa ni ‘mali’ ya Yanga ambayo ilishambulia zaidi lakini wachezaji wake walipoteza nafasi nzuri kufunga.
Kipindi cha pili, Polisi wakaonekana kuimarika na kushambulia zaidi ingawa nao hawakuwa makini katikam ufungaji.
Mliberia, Kpah Sherman naye alionekana kuwa mwiba kwa mabeki wa Polisi.
Hata hivyo beki mkongwe, Lulanga Mapunda aliongoza vizuri safu yake ulinzi ya Polisi kuhakikisha hairuhusu bao tena.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment