Wakazi wa Kimara Baruti Jijini Dar es salaam wapo hatarini kukumbwa na Magonjwa ya Mripuko baada ya eneo wanalohifadhia taka kujaa.
Wakazi hao wamesema kuwa hapo awali walikuwa wakiweka taka hizo katika magari ya kuzolea taka lakini cha kushangaza magari hayo hayapiti hali inayowapelekea kukaa na taka hizo majumbani huku wengine wakizipeleka eneo la kilungule kwa ajili ya kutupa bila kuzingatia kanuni za afya.
Wameongeza kuwa tarari wameshatoa taarifa kwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa ili kutatua tatizo hilo lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ili kuweza kutatua tatizo hilo.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment