“ Jana tar 27 January mwaka huu Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama chaCUFProf.Ibrahim Lipumbaalikuwa na ratiba ya kufanya mkutano wa hadhara pamoja na maandamano… walifuata taratibu zote za kisheria na za kikatiba… La kushangaza dakika za mwisho Jeshi la Polisi walikataza jambo hilo lisiendelee naProf. Lipumbaakaonyesha ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutokuendelea na jambo hilo, lakini Jeshi la Polisi likafika baadae kidogo wakaamua kutumia nguvu dhidi ya raia ambao hawafanyi fujo yoyote, raia ambao walionyesha ushirikiano na utii kwa Jeshi la Polisi, wakaamua kumpigaProf. Lipumba, wakawapiga wanachama na raia wengine wa Tanzania hata watoto wadogo chini ya umri wa miaka 5 wakapigwa mabomu, Waandishi wa Habari wakapigwa virungu kwa kudhalilishwa sana.. jambo hili linaondoa Utulivu, Amani na kuaminiana kwa Taifa letu
Kuwa Jeshi la Polisi lilisema lenyewe jana kwamba ni agizo kutoka juu, tunataka tujue hilo agizo kutoka juu ni kwa nani, kwa sababu gani na kwa maslahi gani? Naomba Mheshimiwa Spika kutoa hoja tuahirishe shughuli za Bunge tulijadili jambo hili kwa maslahi mapana kwa Taifa letu, tulijadili jambo hili ili tuweze kupata majibu sahihi na tuhakikishe kwamba jambo hili halitajitokeza” –James Mbatia.
Akijibu kuhusu ishu hiyo SpikaMakindaakasema;“Ninachosema jambo hili ni kubwa sana, hatuwezi kuzungumza kama mnavyozungumza saa hizi, ni vizuri watu wote wakaelewa tutazungumza na mtoa hojaMbatiatumezungumza akiwepoTundu Lissu, Engineer Mnyaa na ndio mimi nimewaruhusu kwamba hili sualaMbatiaatasema halafu naitaka Serikali nimesema kesho na kesho tutatenga wakati“
Wabunge walionekana kupingana na majibu ya SpikaMakinda, ikatangazwa kuahirishwa kikao hicho; “Naahirisha bunge mpaka saa kumi“– SpikaAnne Makinda.
No comments:
Post a Comment