Wednesday, January 28, 2015

WANANCHI WATAKIWA KUFANYA MABADILIKO YA NAMBA ZA PIKIPIKI WILAYANI LUDEWA KATIKA MKOA WA NJOMBE

Wamiliki wa vyombo vya moto ikiwemo pikipiki, bajaji na magari wilaya yan ludewa mkoani njombewametakiwa kuendelea kufanya mabadiliko ya namba za vyombo hivyo hasa pikipiki zenye namba zinazoanza naherufi T ili zianze na herufi Mc. Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni ofisini kwake meneja wa mamlaka ya mapato TRA wilaya ya ludewa mkoani njombebw, Mro nyattahalisema kuwa zoezi hilo limeanza tangu tarehe1 octoba mwaka jana na litaisha tarehe 31 mwezi wa 3 mwaka huu huku akisema wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya usalama wa vyombo vyao kwani namba nyingi za pikipiki zinaingiliana na namba za magari. Aidha alisema kuwa mmiliki wa pikipiki anatakiwa kufika na kadi Halisi ya pikipiki, kopi ya tini namba pamoja na pikipiki yenyewe katika ofisi za TRA wilaya ya ludewa kwa ajili ya kufanya mabadiliko hayo. Alisema kwa mmiliki wa chombo cha moto aliyekidhi vigezo kama kadi halisi ya pikipiki na tini atafanya mabadiliko hayo kwa kulipa kiasi cha shilingi elfu kumi za kitanzania na kwa yule ambae hana vitu hivyo atalazimika kusafiri kwenda makao makuu ya TRA Mkoani Iringa kwaajili ya kufanya mabadiliko hayo. Hatahivyo aliongeza kuwa muda uliobaki nimchache sana hadi kukamilisha zoezi hilo hivyo uongozi wa TRA utalazimika kuongeza muda kwaajili ya kuwasaidia wamiliki wa vyombo hivyo kufanya maboresho hayo kwa wingi zaidi. Pia aliwataka wamiliki wa vyombo vya moto wilayani ludewa kutumia ipasavyo muda uliobaki kwaajili ya kufanya mabadiliko ya vyombo vyao ili kujiepusha na usumbufu unaoweza kujitokeza mara baada ya muda uliopangwa kuisha.

No comments:

Post a Comment