Majambazi wapiga na kupora bunduki na risasi polisi

Ikiwa ni wiki moja Tangu polisi kuporwa bunduki na kuuwawa huko Ikwiriri, janga hili limeendelea tena pale watu wanaosadikiwa ni majambazi kuwapiga na kuwapora bunduki na risasi askari huko jijini Tanga. Kwenye tukio hilo lililotokea barabara ya tano huko Tanga baada ya Askari waliokuwa wakitoka kula chipsi kuvamiwa na majambazi na kupata kichapo kikali kabla ya kuamuliwa kuachia Bunduki. Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Juma Ndaki amesema katika tukio hilo ambalo askari PC Masoul alichomwa kisu na akapelekwa haraka kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga. Pia amesema upelelezi unaendelea ili kubaini watu waliofanya tukio hilo ila mpaka sasa ajapatikana mtu yoyote anaehusika na uporaji huo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: