Mahakama ya wilaya ya ludewa mkoa wa njombe imewasomea mashitaka watuhumiwa watatu pamoja na aliyekuwa askari wa jeshi la polisi wa kituo cha ludewa mjini mwenye namba G, 6352 Abduel Amza Nyuki mwenye umri wa miaka 3o,Juma mhagama 21 pamoja na Rashidi amadi wote wakazi wa mtaa wa ibani ludewa mjini kwa kesi ya mauwaji kinyume na kifungu cha sheria cha 196 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kesi hiyo imesomwa January 26 na Wakili Edward Mohamed mtahiruka mbele ya hakimu wa wilaya Fredrick lukuna na kusema kuwa tukio hilo lilifanyika usiku wa kuamkia january 23.2015 majira ya saa sita kamili usiku katika mtaa wa mdonga wilayani Ludewa ambapo watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa kosa la Mauaji ya January mtitu aliyekuwa na umri wa miaka 20.
Wakili huyo alisema kuwa Aliyekuwa askari wa jeshi lapolisi ludewa mjini Bw, Abduel Nyuki ndiye aliye kuwa muhusika wa kufanya ,auaji hayo kwa kutumia risasi mnamo usiku wa kuamkia january 23 saa sita usiku kwakuambatana na vijana hao wawili ambao walimpeleka mtuhumiwa huyo nyumbani kwa marehemu na kwenda kufanya mauaji hayo.
Hata hivyo watuhumiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote na kuwa keso hiyo imeahirishwa hadi tarehe 2.2.2015 Hivyo watuhumiwa wamerudishwa mahabusu kwakuwa kesi yao haina mdhamana.
Home
Uncategories
HUKUMU YA POLISI ALIUWA KWA RISASI LUDEWA YASIKIKILIZWA KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA;
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment