FILIKUNJOMBE AWATIMIZIA AHADI YA MAJI WANANCHI WA KITEWELE ZAIDI YA TSH MILIONI 26 ZATUMIKA
WANANCHI wa Kijiji cha KITEWELE kata ya MAWENGI wilaya ya LUDEWA mkoani Njombe , wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama ya bomba baada ya kukamilika kwa ununuzi wa vifaa ikiwemo mabomba ya kutandika ardhini ambayo yamegharimu kiasi shilingi zaidi ya Milioni 26 msaada uliotolewa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe .
Akizungumza leo na wananchi hao mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo mbunge Filikunjombe alisema kuwa kukabidhi kwa vifaa hivyo na mradi huo wa maji ni utekelezaji wa ahadi yake ya maji kwa wananchi hao aliyoitoa mwaka 2012 kufiatia ombi la wananchi hao zaidi ya 800 waliokuwa wakikabiliwa na adha ya maji .
Mbunge Filikunjombe alisema kuwa toka nchi itape uhuru mwaka 1961 wananchi hao hawajapata kuwa na maji safi na salama na kuwa miaka yote wamekuwa wakitumia maji ya mito ambayo si safi na salama kabla ya kufika na kuombwa kuwasaidia kupata huduma hiyo ya maji safi .
“Ndugu zangu nikiwa kama mbunge wenu nimekuwa nikiumia zaidi kuona wananchi wangu mnapata shida ya maji na ndio sababu ya kuahidi kuungana nanyi katika kuwafikishia huduma ya maji….ombi langu kwenu tuzidi kushirikiana ili kutatua kero zetu bila kusubiri wahisani “
Miaka miwili iliyopita, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, DEO FILIKUNJOMBE alishuhudia kadhia hiyo akiwa katika Zahanati ya kijiji hicho na akawaahidi wananchi kuwafikishia maji, ahadi ambayo ameitekeleza mwaka huu na kukabidhi mabomba kwa wananchi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 tayari kwa kuanza kazi ya kuchimba mitaro na kutandika mabomba hayo.
Hata hivyo alisema kuwa maendeleo ya wananchi wa KItelewe na jimbo la Ludewa yataletwa na wananchi wenyewe kwa kuunganisha nguvu zao pasipo kusubiri wahisani na kuwa baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo wananchi siku zote wamekuwa wakijitolea kushiriki katika maendeleo mbali mbali.
Akielezea kuhusu adha ya maji katika jimbo lake na jinsi alivyoshiriki kutatua alisema kuwa yapo maeneo ambayo wananchi wamekuwa na adha kubwa ya maji na tayari ameanza kumaliza kero hiyo.
Kwa upande wake diwani wa viti maalum tarafa ya Mawengi Bilgeter Haule aliema kuwa moja ya vitu ambavyo wana Ludewa wanajivunia ni kumpata mbunge ambaye anawajibika kwa wananchi kama ilivyo kwa mbunge huyo.
“ Tanzania mtu ambae hatakuj kusaulik ni pamoja na baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere ambae alitanagazwa kuwa mwana heri ila kwetu Ludewa kutokana na kero tulizozipata toka uhuru hadi leo ambapo zinapatiwa ufumbuzi kwa pamoja tutamkumbuka mheshimiwa mbunge wetu Deo Filikunjombe kama mwanaheri baada ya kutatua kero zetu na kuondoka katika kundi la watanzania wasiofurahia uhuru wao”
0 comments:
Post a Comment