BWANA HARUSI AFARIKI DUNIA DAKIKA CHACHE KABLA YA KUFUNGA NDOA

Sherehe moja kubwa ya harusi iliyopangwa kufanyikaTurkana, Kenyailiingia majonzi makubwa saa chache kabla ya sherehe hiyo kufanyika. Binadamu tumekuwa tunapanga mengi kwenye maisha wakati Mungu anapanga yake pia, yale yote yaliyopangwa kufanyika siku ya Harusi hiyo ikiwemo kukata keki pamoja na burudani ya waimbaji wa kwaya, ililazimika yafanyike siku ya msiba waPeter Erooambaye ilikuwa awe Bwana Harusi kwenye ndoa hiyo huku ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye simanzi kubwa. Bibi harusiPerpetua Abenyoalikuwa kwenye wakati mgumu lakini hakuwa na jinsi ya kupingana na ukweli kwamba mtu aliyekuwa awe mume wake hakuwa naye tena, mauti yalimkuta Jumamosi iliyopita baada ya kuugua ghafla na kufariki saa chache kabla ya ndoa yao. Mazishi yaPeteryalifanyika jana December 12,Perpetuaakisema imani yake haitoyumba na anaamini kila kitu ni mipango ya Mungu.Unaweza kuisikiliza Habari ambayo nimekurekodia kutokaCitize Tv pamoja nakuangalia video ya taarifa hiyo na kuitazama.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: