ZAMBIA SARE 1-1 NA DRC AFCON

ZAMBIA imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 leo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi B Fainali za Mataifa ya Afrika zilizoanza jana nchini Equagorial Guinea.
Given Singuluma alitangulia kuifungia Chipolopolo dakika ya pili ya mchezo, kabla ya Yannick Bolasie kuisawazishia DRC dakika ya 66.
Mechi nyingine ya Kundi hilo, kati ya Tunisia na Cerpe Verde itaanza Saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Mechi za ufunguzi jana, Gabon ilijiweka kileleni mwa Kundi A kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso.
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang, aliifungia Gabon bao la kwanza dakika ya 19, kabla ya Malick Evouna kufunga la pili dakika ya 72.
Gabon sasa inaanza na pointi tatu kileleni mwa kundi, mbele ya wenyeji Equatorial Guinea wenye pointi moja sawa na Kongo baada ya sare ya 1-1 baina yao, wakati Burkina Fasso inashika mkia ikiwa haina pointi.
Bao la dakika ya 87 la Bifouma Koulossa liliinusuru Kongo kulala mbele ya Equatorial Guinea, baada ya Nsue Lopez kutangulia kuwafungia wenyeji dakika ya 16.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: