TAZAMA KILICHOANDIKWA FACEBOOK KUHUSIANA NA RAIS JAKAYA KIKWETE
RAIS KIKWETE
HAYA NI MAONI YA WANANCHI KWENDA KWA MHE JAKAYA KIKWETE KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK JINSI WATU WANAVYOENDELEA KULIONGELEA SWALA LA ESCROW
Iddy Harnaa Mkwama
Hili shinikizo la kumtaka Rais achukue hatua za haraka kuwawajibisha watendaji wake linanipa mashaka, linanifanya nianze kuamini yale yanayosemwa kwamba kuna vita binafsi zimeingizwa kwenye sakata la ESCROW, ripoti imekabidhiwa kwa Rais, kuna vyombo vimepewa jukumu la kuchunguza baadhi ya mambo kisha vitoe majibu na hatua zichukuliwe, haraka ya nini? Mbona wengine walipewa muda wa kuchunguza na kufuatilia kwanini wengine nao wasipewe muda?
Goodluckies Good
Mhe. Rais, tunakuomba ufanye maamuzi haraka juu ya waliohusika ama moja kwa moja, ama kwa makosa ya kiuongozi na maadili, katika hili sakata la ESCROW, kabla wananchi hatujaamua kufanya maamuzi halafu na liwalo na liwe, maana hii inamaanisha hivi sasa tunasubiri hili lipoe halafu liibuke lingine, hatutaki upinzani usio na tija, sisi ni wananchi tunaoumia na maisha ya kila siku, wewe hapo ikulu hata soksi hujui kuwa imeisha, anayejua ni mwengine, wewe ni kuweka miguu juu tu.
Tafadhali sana Mheshimiwa, tunza heshima yako kwa kufanya maamuzi magumu juu ya hili. Hebu ona, umeondoka juzijuzi tu kwamba unaumwa, umeenda kutibiwa marekani, umerudi ukaanza kujibalaguza kwa kuwasifia madakitari wa marekani namna wanavyofanya kazi yao kwa weledi mkubwa na kwa taaluma ya juu kabisa, kutuaminisha kuwa Tanzania madakitari wetu bado sana, na elimu yetu itasubiri sana. Ukaendelea kutuzuga na stori za kuhusu ugonjwa wa tezi dume, sawa, tumekaa kimya, sasa umerudi na ni kama wiki sasa imeyoyoma, umekaa kimya, tuamini nini? ulikimbia ile skendo kwenda marekani kusubiri iishe ndo urudi? please, tunakusubiri, na utuambie tukupe siku ngapi ili ufanye maamuzi hayo haraka iwezekanavyo.
Na mwananchi mtiifu.—.
Malisa Godlisten
Ukimya wa Rais Kikwete ktk kutekeleza mapendekezo ya bunge kunanifanya niamini habari zilizoenea kuwa familia yake (JK) ilihusika na wizi wa fedha za Escrow.!
Mdude Chadema Nyagali
·
ESCROW kuna siri kubwa kati ya rais kikwete na James Rugemalira na seth wamiliki wa IPTL na PAP kitendo kinachomfanya rais kushindwa kuyafanyia kazi maamuzi ya bunge.
kuna taarifa kuwa mmoja wa wanafamilia wa rais amechukua bilion 5 pesa za ESCROW kwa hiyo James Rugemalira na Seth Singh wamekuwa ndio washauli wa rais kikwete kuhusu suala hili na kikwete anaufanyia kazi ushauri wa wezi hawa badala ya ushauli wa bunge kwa kuwa anajua moja ya familia yake wanahusika.kuna mawasiliano ya karibu kwanjia ya imeil na simu kati ya rais na hawa wezi wa ESCROW.
hivyo basi na James Rugemalira ndio waliochukua nafasi ya bunge kuishauri serikali na rais anaufanyia kazi kwa maana hiyo bunge halina kazi tena kwa kuwa serikali haifanyii kazi tena ushauri wa bunge na ndio maana ata rais umeona yuko kimya tangu bunge liazimie wezi wa ESCROW wachukuliwe hatua pamoja na kwamba nchi wahisani wamegoma kutoa misaada kwa sababu ya wezi hawa.
tusikubali James Rugemalira na Seth Singh wawe ndio wawe washauri wa serikali badala ya bunge,yani fisi awe mshauri wa mwenye bucha?
watanzania mpaka sasa tusitegemee rais kuufanyia kazi ushauri wa bunge kwa kuwa amelidharau hivyo sisi wananchi wabunge na viongozi wa vyama vya upinzani kumlazimisha rais aufanyie kazi ushauri wa bunge .—
Malisa Godlisten
Nadhani JK akisikiliza wimbo huu anaweza kuchukua maamuzi ya wale jamaa wa Escrow."Waite Waite ite ite, wakalishe chini kwanza, watoe hofu kwanza, wambie wao hawamo japo nao walikula" Mrisho Mpoto.
Zawadi Beatus Lupelo
Wakati akitoa mchango wake bungeni mh Tundu Lissu bungeni kuhusiana na escrowsaga alijaribu kuhusisha historian ya hili sakata lilivyoanza na historian ya kiuongozi ya mtu aliyemtaja kama kanali jakaya mrisho kikwete ambaye ndiye Rais wa Tanzania. Ingawa wabunge wenzie hawakupenda bado tena mbunge David Kafulila amerudia kusema familia ya Rais inahusika kwenye wizi wa fedha za escrow. Huenda tuhuma hizi zisiwe za kweli lakini ukimya wa Rais ktk hili na kuchelewa kwake kutekeleza maazimio ya bunge kunaleta maswali akilini mwangu juu ya kutohusika kwa Rais. Nikirejea mchango wa mtoto wa Rais bungeni mh Ridhiwani Kikwete kuwa hela za escrow siyo za serikali naishiwa maneno ya kuandika.
Mutalemwa Zakalia
KWANINI Mh.Rais JAKAYA KIKWETE AMEKUA MZITO KWENYE JAMBO LA {escrow?}
Thadei Ole Mushi
Mh Raisi sisi wazelando wa nchi hii wenye uchungu na nChi hii, tunaojua ilikotokea na inakoelekea.
Tunamhitaji sana Mhongo kuliko mtu mwingine kwa sasa tunakoelekea kuwa wazalishaji wa gesi na mafuta.Tunakuomba usimfukuze kazi mh Raisi
0 comments:
Post a Comment