RAIS WA ZAMANI WA MAREKANI ALAZWA

Aliyekuwa rais wa Marekani George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali moja ya Houston nchini Marekani baada ya kupatikana na tatizo la kupumua. Kwa mujibu wa madaktari, Bush mwenye umri wa miaka 90 anachunguzwa katika hospitali ya Methodist. Alipelekwa katika hospitali hiyo na kwa gari la wagonjwa jumanne usiku. Wawakilishi wa Bush wanasema kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari. Rais huyo wa 41 ndio mzee zaidi kuwahi kuiongoza nchi ya Marekani. Bush ambaye hawezi kutumia miguu yake, hivi majuzi alionekana amekaa katika kiti cha magurudumu katika hafla iliofanyika mwezi November katika chuo kikuu cha Texas.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: