JAMII YAASWA KUTOWAFICHA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO

Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharibu Bilal amewataka wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kuwaficha majumbani watoto wanaobainika kuwa na matatizo ya moyo. Akizungumza jijini Dar es saalam wakati akiwaaga watoto hamsini na tano wenye matatizo ya moyo wanaopelekwa nchini india kwa matibabu Dr.Bilal amesema kuwa serikali inaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha inapunguza vifo vitokanavyo na matatizo hayo. Naye mlezi wa watoto wanaopelekwa nchini india mbali na kutoa shukrani zao kwa wafadhili wa safari hiyo wametoa wito kwa wadau wengine kuendela kuongeza nguvu ili kuwasaidia watoto wengi zaidi. Katika hatua nyingine wahisani waliofanikisha safari hiyo wamesema wataendelea kupambana na tatizo hilo linaloendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitolea.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: