NSSF YADHAMINI MASHINDANO YA SHIMISEMITA MKOANI MOROGORO

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ndio mdhamini Mkuu wa mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (Shimisemita) inayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro hadi Novemba 11. Katika mashindano hayo NSSF imepata fursa ya kutoa elimu kuhusu Mafao mbalimabli yatolewayo na Shirika hilo ikiwemo Mango mpya kwa ajili ya Wakulima na Wachimbaji wadogo wa Madini. Katika mpango huo, Wakulima sasa wanaweza kujiunga na NSSF na kufaidika na Mafao mbalimbali yanayotolewa na NSSF. Pia Wakulima wanaweza kufaidika na mikopo mbalimbali ikiwemo mikopo ya pembejeo na Vifaa. Vilevile wakazi wa Mkoa wa Morogoro na wale kutoka Halmashauri mbalimbali Nchini wanaweza kupata elimu kuhusu uchangiaji wa Hiari, Kupitia Mpango huu. Wote walio katika sekta isiyo rasmi, wafanyakazi, wafanyabiashara wanaweza kujiunga na NSSF na kufaidika na Huduma mbalimbali kama vile Mafao ya Matibabu na Mikopo kupitia SACCOS.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: