Jeshi lagawanyika kuhusu uongozi B.Faso

Mgawanyiko umeripotiwa ndani ya jeshi la Burkina Faso kuhusu ni nani anayefaa kuliongoza taifa hilo kufuatia kujiuzulu kwa rais Blaise Campaore baada ya miaka 27 uongozini. Kituo kimoja cha radio kilitangaza taarifa kutoka kwa naibu mkuu wa kikosi cha kumlinda rais kanali Isaac Zida iliyosema kuwa amechukua jukumu la kuliongoza taifa hilo. Mapema mkuu wa majeshi Honore Traore alitangaza kuwa alikuwa amechukua usukani Jen.Honore Traore Blaise Compaore alijiuzulu baada ya kushuhudia maandamano yenye ghasia baada ya jitihada zake za kutaka kuliongoza taifa hilo kwa awamu nyengine kupitia bunge kugonga mwamba. Akizungumza hapo jana kanali Zida amesema kuwa Jenerali Traore hawezi kuliongoza taifa hilo. ''Nimechukua jukumu la kuliongoza taifa hili na serikali ya mpito ili kuliendeleza na kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya kidemokrasia kwa njia ya amani'' alisema kanali Zida katika hotuba yake katika runinga. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: