ASKOFU MALASUSA AONGOZA MAZISHI YA ASKOFU LUKILO WA KKKT NJOMBE.
ASKOFU MALASUSA AONGOZA MAZISHI YA ASKOFU LUKILO WA KKKT NJOMBE.
Njombe.
ASKOFU wa kanisa la kiinjili la kirutheli Tanzania KKKT, Alex Malasusa hapo jana amewaongoza waumini wa kanisa hilo na wananchi wengine katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa askofu mstaafu wa awamu ya nne Marehemu Cleopa Akutulaga Lukilo ambaye alifariki novemba 13 nyumbani kwake na kuzikwa hapo jana katika viwanja vya kanisa hilo mjini Njombe.
Akihibiri katika mazishi hayo yaliyofanyika katika kanisa la kilutheri Dayosisi ya kusini Njombe Askofu Malasusa aliwataka wananchi kuacha kufuatilia tofauti zao badala yake kuuutumia mda huo kufanya shughuli za maendeleo na kuwasaidia masikini na wenye matatizo.
Aidha Malasusa aliwasihi waumini wa kanisa hilo kuepukana na tabia za kulipiza visasi na kutafuta riziki kwa njia halali na sio kwa njia ya udanganyifu na kujenga mazoea ya kutubu dhambi kwa sababu mwanadamu hajui saa wala dakika ya kufariki kwake.
"natamani tungekuwa tunaamani muda wote lakini amani haiwezi kuwepo bila ya watu kutengeneza bila watu kutubu dhambi tujifunze kutubu dhambi kwa sababu hakuna anayejua siku ya kufa anayejua ni mungu pekee inatubidi tujiandae siku zote kwa kutubu" alisema Malasusa.
Alisema kuwa marehemu alifariki siku nne baadae baada ya kusema kuwa yeye amejiandaa kufa wakati akifungua mkutano wa umoja wa wanawake wamakanisa mkoani Njombe.
Alisema kuwa marehemu alitaja mara nne kuwa anejiandaa kuwa akisema"Mimi nimejiandaa kufa, mini nimejiandaa kufa vizuru" alisema wakati wa kufungua mkutano huo na kufa siku nne baadae.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk. Rehema Nchimbi akitoa salamu za rambirambi aliwataka waumini wa kanisa hilo kutoka mkoa wa Njombe kuendelea kumuenzi kwa kufuata mema aliyoyafanya marehemu Askofu katika kulitumikia kanisa hilo ikiwemo kuanzisha chuo cha kikuu cha Tumaini tawi la Amani la Njombe.
Aliwasihi viongozi wa kanisa hilo kuendelea kutumikia vizuri nafasi za utumishi walizonazo na kuongeza bidii kuliombea Taifa la Tanzania ili kujengeka kiimani na watulivu.
"Huu ni wakati mgumu sana sote tunatakiwa kuungana kunzia nyinyi viongozi wa kanisa kwa ngazi zote kuendelea kuliombea taifa ukiwemo Mkoa wetu ili tuwe na amani siku zote na tuwe mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na amani" alisema Nchimbi.
Dr. Nchimbi alisema kuwa viongozi wanatakiwa kuombewa ili wasiweze kutafuna mali za umma na kuwa watiifu wanapokuwa katika uongozi wa wananchi mpaka wanamaliza mda wao wa kuongoza kwani viongozi hao ni moja ya kondoo wanao wachunga.
Akisoma historia ya marehemu, Katibu mkuu wa dayosisi ya kusini Timias Mhomisoli alisema kuwa Askofu Lukilo alizaliwa mwaka 1949 katika kijiji cha ukemele wilayani Mufindi Mkoani Iringa na kufariki novemba 13 mwaka huu, maiti yake kuzikwa hapo jana katika viwanja vya kanisa kuu la dayosisi ya kusini Njombe.
....END.
0 comments:
Post a Comment