TAARIFA MPYA KUTOKA MOSHI KUHUSU MGONJWA WA EBOLA
Serikali mkoani kilimanjaro imewaondoa hofu wananchi kwa kupinga taarifa za uwepo wa ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa tishio kwa nchi za aArika kufuatia taarifa za kugundulika kwa mgonjwa mwenye Dalili za ugonjwa huo katika kituo cha afya Shirimatunda manispaa ya Moshi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama amesema mgonjwa huyo amepelekwa katika kituo hicho kilichotengwa kwa ajili ya wagonjwa watakaogundulika kuwa na viashiria vya ugonjwa huo kutokana na histori ya mgonjwa huyo ambaye alikuwa na homa kali kuonyesha alikuwa ametokea nchini Senegal.
Amesema mgonjwa huyo kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba vipimo vya awali vimeonyesha mgonjwa huyo alikuwa na ugonjwa wa maleria na kwamba tayari ameshatolewa sampuli na kupelekwa jijini Dar es salaamu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako amewataka wananchi kuchukua tahadhari za kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuepuka salamu za kushikana mikono.
Nao baadhi ya wananchi wa manispaa ya moshi wameiomba serikali kutoa elimu zaidi kwa wananchi juu ya ugonjwa huo na kuchukua tahadhari za kukabiliana na wageni wanaoingia hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment