MAHAKAMA YA WILAYA YAWASOMEA MASHTAKA WASHTAKIWA WA MAKOSA YA MAUAJI KWAAJILI YA KESI ZAO KUSIKILIZWA NA MAHAKAMA KUU

Mahakama Ya Wilaya Ya Njombe Leo Imewasomea Mashtaka Washtakiwa Mbalimbali Wa Makosa Ya Mauaji Kwaajili Ya Kesi Zao Kupelekwa Kusikilizwa Katika Mahakama Kuu Ambapo Miongoni Mwa Washtakiwa Ni Pamoja Na Jason Swale Mkazi Wa Kijiji Cha Makolango Makambako Anayeshtakiwa Kwa Kosa La Kumuua Anastanzia Mangula. Washtakiwa Wengine Ni Pamoja Na Jofrey Nyava Ambaye Anatuhumiwa Kumuua Baba Yake Joshuwa Nyave Mkazi Wa Kijiji Cha Igwachanya,James Msumule Maarufu Kwa Jina La Jembe,Emmanuel Ngairo Maarufu Kwa Jina La Emma,Isack Ngairo,Anitha Mbwilo;Upendo Mligo Ambao Wote Kwa Pamoja Wanatuhumiwa Kwa Kosa La Kumuua Alice Mtokoma Mkazi Wa Kijiji Cha Usalule Wilayani Wanging'ombe. Akisoma Hati Ya Mashtaka Na Maelezo Ya Mashahidi Watakaokwenda Kutolea Ushahidi Wao Na Vielelezo Katika Mahakama Kuu, Wakili Wa Serikali Riziki Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa Mshtakiwa Geofrey Nyave Alitenda Kosa Hilo Mnamo April Mwaka 2012 Ambapo Alifanya Kosa La Mauaji Ya Kukusudia Kumuua Baba Yake Joshuwa Nyave Kinyume Na Kifungu Cha 196 Na 197 Cha Sheria Ya Kanuni Za Adhabu Sura Ya 16 Ya Marejeo Ya Mwaka 2002. Wakili Matiku Amewataja Watuhumiwa James Msumule,Emmanuel Ngairo,Isack Ngairo,Anitha Mbwilo Na Upendo Mligo Wakazi Wa Kijiji Cha Usalule Kuwa Walitenda Kosa Hilo Kwa Kumuua Alice Mtokoma Wakimutuhumu Kwa Imani Za Kishirikina Kinyume Na Kifungu Cha 196 Na 197 Cha Sheria Ya Kanuni Ya Adhabu Sura Ya 16 Ya Marejeo Ya Mwaka 2002. Aidha Wakili Matiku Amemtaja Mtuhumiwa Castori Chatanda Mkazi Wa Kijiji Cha Iboya Kuhusika Na Mauaji Ya Marehemu Sebastian Chatanda Yaliotokea July 2013 Kuwa Ni Mauaji Ya Kutokukusudia Kinyume Na Kifungu Cha 195 Na 198 Sura Ya 16 Ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2002. Hakimu Wa Mahakama Ya Wilaya Ya Njombe Augustine Rwizile Amesema Washtakiwa Hawaruhusiwi Kujibu Chochote Dhidi Ya Makosa Hayo Hadi Hapo Mashtaka Hayo Yatakapo Fikishwa Katika Mahakama Kuu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: