VETERANI COMBAIN YAWAONYESHA KIPAJI VIJANA WA KIPANGALA FC
Mchezo wa Ligi ya Kuambiana Cup, unaoendelea katika Tarafa ya Masasi, Wilaya ya Ludewa, umemalizika kwa timu ya Veterani Combain kuwashinda vijana wa Kipangala FC kwa mabao 2–1.
Mchezo huo umeonyesha uzoefu na ubora wa wachezaji wa zamani, ambao licha ya umri wao, waliweza kuwazidi maarifa vijana wa Kipangala. Veterani hao wamethibitisha kuwa wao ni hazina kwa soka la kizazi kipya, wakionesha mbinu na ustadi wa hali ya
juu katika kusakata kabumbu.
Tazama vilivyomo na matangazo
Ludewa yetu na maendeleo yetu
posted by barnabas njenjema,
kutoka Ludewa
No comments:
Post a Comment