Wahudumu wa Mochwari katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wamegoma kuzika miili ya watu iliyoharibika kufuatia hospitali hiyo kushindwa kuwalipa mishahara yao.
Aidha, wahudumu hao ambao ni tisa walisema jana kuwa tangu mwezi juni mwaka jana hadi sasa hawajalipwa mishahara yao licha ya kufikisha madai yao katika uongozi wa hospitali hiyo na halmashauri ya wilaya ya Bariadi.
Wahudumu hao Walisema katika madai yao, wanaidai hospitali hiyo zaidi ya Sh milioni 2 huku wakibainisha kuwa kila mmoja anadai Sh 260,000 kwa ajili ya malipo ya kazi wanayofanya ya maziko.
Kwa upnde wa Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Godfrey Mpangala, alikiri kuwapo kwa madai ya wahudumu hao na mgomo huo na kubainisha kuwa tatizo lilitokana na Serikali kutopeleka fedha za matumizi mengine suala lililopelekea kushindwa kuwalipa wahudumu hao
No comments:
Post a Comment