Msanii wa kundi la Tip Top Connection, Hamad Ally “Madee”, amefichua siri ya wasanii kutofanya vizuri na kusema kuwa ni kutokana na kurekodi nyimbo mfululizo na ndio maana hawafanyi kwa ufasaha.
Amesema kuwa wasanii wanatakiwa kujipa muda ili kuweza kupika vitu vizuri vyenye radha ambayo haiwezi kuwakinai wasikilizaji na kuongeza kuwa wanatakiwa kuna na mawazo mapya na sio kuwa na wazo la aina moja.
Amesema kwa upande wake amejipanga baada ya kurekodi wimbo wa sasa atakupumzika kwa muda wa miezi sita ili kuweza kuona kipi aongeze katika kazi inayofuata na maneno gani ambayo atayatumia kwa wakati ambao atahitaji kutoa ngoma mpya.
No comments:
Post a Comment