Mwanasayansi wa zamani katika mahabara ya kitaifa mjini Los Amos nchini Marekani amefungwa jela miaka mitano kwa kujaribu kuipatia nchi ya Venezuela siri za kutengeza bomu la nyuklia.
Pedro Leonardo Mascheroni alikiri kosa mwaka 2013 la kutoa siri kwa jasusi wa FBI aliyejidai kuwa afisa mkuu kutoka Venezuela. Pedro Mascheroni, mwenye umri wa miaka 79,anatoka nchini Argentina pamoja na Mkewe pia alifungwa jela mwaka mmoja.
Mascheroni alikuwa anachunguzwa kwa karibu mwaka mmoja kabla ya kuchukuliwa hatua. Shirika la ujasusi la FBI, lilinasa komputa, barua , picha na vitabu kutoka nyumbani kwa mwanasayansi huyo.
Kulingana na stakabadhi za mahakamani, bwana Mascheroni aliambia afisaa huyo wa FBI kwamba angeweza kuisiadia Venezula kutengeza bomu la nyuklia kwa kipindi cha miaka kumi.
Alisema nchi hiyo ingeweza kutengeza mtambo wa kisiri wa nyuklia chini ya ardhi kuisiaidia kurutubisha madini ya Plutonium.
Bwana Mascheroni alifanya kazi kwa karibu miaka kumi katika kitengo cha kutengeza zana za nyuklia katika mahabara ya kitaifa ya Marekani ambako bomu la kwanza la Atomiki lilitengezwa.
Aliachishwa kazi mwaka 1988. Mkewe alikuwa mwandishi wa maswala ya teknolojia katika mahabara hio.
No comments:
Post a Comment