Na njenje ze ropo
Ludewa sport
Kwa mwaka huu, mashindano haya yameingia msimu wake wa sita, yakihusisha jumla ya timu 23 kutoka maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Masasi. Kuambiana Cup ilianzishwa kwa lengo la kukuza vipaji, kuhamasisha mshikamano wa kijamii na kuleta maendeleo kupitia michezo, chini ya mwanzilishi wake na mlezi wa mashindano haya, Ndugu Iman Abed Haule Kuambiana, Mkurugenzi wa Kuambiana Investment Company Ltd.
Katika mchezo wa ufunguzi, timu ya SHUMA FC, mabingwa watetezi, walikutana na wapinzani wao wakuu Mbongo FC, waliomaliza nafasi ya pili msimu uliopita. Mchezo huo wa kuvutia ulimalizika kwa Mbongo FC kuibuka kidedea kwa mabao 2–0, na hivyo kutwaa Ngao ya Hisani kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya.
Mbongo FC walionyesha kiwango cha juu cha mchezo, wakitawala sehemu kubwa ya mchezo na kutumia vizuri nafasi zao. Ushindi huo umeweka historia mpya na kuongeza motisha kwa timu nyingine kushiriki kwa ushindani mkubwa.
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Olvanus Paul Thomas, ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Ndugu Sunday Deogratias, pamoja na viongozi wengine wa serikali, michezo na jamii.
Kwa pamoja, walimpongeza kwa dhati Ndugu Iman Haule Kuambiana kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha michezo na kuleta hamasa ya maendeleo ndani ya Tarafa ya Masasi kupitia mashindano haya.
Pia waliomba wadau Zaid waweza kujitokeza kushirikiana na kuambiana kudhamin mashindano haya mpaka sasa mashindano haya yanadhaminiwa na CRDB bank.
0 comments:
Post a Comment