Saturday, June 7, 2025

Jogging Yazinduliwa Rasmi Ludewa – Wananchi Wajitokeza kwa Wingi, Michezo Yasisimua


Na @njenjeropo
Ludewa
Wilaya ya Ludewa imeandika historia kwa mara ya kwanza kwa kuzindua rasmi vikundi vya jogging katika hafla ya kipekee iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mheshimiwa Olivanus Thomas, siku ya Jumamosi tarehe 7 Juni 2025, katika uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Uzinduzi huo ulitanguliwa na mazoezi ya pamoja ya alfajiri yaliyoanza saa 11:00 asubuhi, ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio, matembezi na mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya na kuhamasisha utamaduni wa kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
Mbali na mazoezi, shughuli hiyo iliambatana na michezo mbalimbali ya burudani na kijamii, ikiwemo mbio za magunia, mbio za yai kwenye kijiko, kuvuta kamba, mchezo wa kuzunguka kiti na kutambua rangi. Washindi wa michezo hiyo walizawadiwa zawadi mbalimbali kama sehemu ya kutambua juhudi na ushiriki wao.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Olivanus aliwashukuru wananchi kwa mwitikio mkubwa pamoja na wadau wa maendeleo waliofanikisha tukio hilo. Aliwataja baadhi yao kuwa ni Ndg.Iman Abed Kuambiana, Dkt. Philip Philikunjombe na Mheshimiwa Joseph Kamonga.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa wananchi kujiunga na vikundi vya jogging kama njia ya kuimarisha afya, kukuza mshikamano wa kijamii na kujenga ushirikiano kati ya viongozi na wananchi.
Baadhi ya vikundi vilivyozinduliwa rasmi katika hafla hiyo ni pamoja na:
Bomani Jogging Club
Nchuchuma Jogging Club
Liganga Jogging Club
Mafundi Jogging Club
Samia Queens Jogging Club
Usalama Jogging Club
Walimu Jogging Club
Uzinduzi huu umeibua ari na hamasa mpya miongoni mwa wakazi wa Ludewa kuhusu umuhimu wa mazoezi ya mwili, na kutajwa kuwa mwanzo mzuri wa mabadiliko chanya katika mtazamo wa jamii kuhusu afya na maisha bora.
@olivanus_paul_thomas
@phil_kunjombe
@josephzachariuskamonga
@kuambiana_investment_co_ltd









Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa

No comments:

Post a Comment