Monday, August 22, 2016

Jinsi ya kupika uji wa NGANO




Mahitaji:
 Ngano nzima 1/2kg 
Nazi kubwa 2 au 
maziwa yaliyochemshwa 1 litre 
Hiliki kijiko 1 iliyotwangwa 
Unga wa ngano 1/4kg 
Sukari 1/2 kg

Matayarisho:
1.     Chemsha ngano zako mpaka ziwive,
2.    kuna nazi na ichuje tuwi zito, au
3.     tumia maziwa tekeka
4.    sufuria yako ikiwa na maji kiasi,
5.    subiri yachemke,
6.     koroga unga wa ngano na maji baridi kwenye kikombe saiz ya uji.
7.     mimina kwenye sufuria ya maji ya moto.
8.    Huku ikiwa katika moto
9.     koroga ili uji usifanye madonge,
10.  baada ya muda kiasi mimina ngano zako koroga zisifanye madonge ukiona zimeshachanganyika.
11.                       tia sukari na hiliki pamoja na
12.                      tui lako au
13.                      maziwa
14.                      wacha ichemke kama dakika 5.
15.                       Epua ,
16.                      mimina kwenye chupa ya chai.
17.                      Tayarisha vikombe tayari kwa kuliwa.
Muda mzuri jioni hasa siku za baridi.




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa

No comments:

Post a Comment