WANANCHI MUNDINDI LUDEWA WALIA NA ELIMU YA BURE

Wananchi waishio
kata ya mndindi kijiji cha amani wilayani ludewa mkoani njombe wamemtaka katibu
wa ujenzi bw Linus Kayombo kuwapa
takwimu ya mapato na matumizi ya mwaka
jana yaliyo tumika kujengea moja ya
jengo la darasa la shule ya sekondali ya mndindi. Wakizungumza na
radio best fm mwenyekiti na afisa mtendaji wa kijiji hicho wamesema kuwa awali
walichagua kamati ya ujenzi ya madarasa ya shule ya hiyo ya sekondari amabapo
wanashangaa kutopata takwimu ya mapato na matumizi ya mwaka jana ya ujenzi wa
madarasa hayo na hivyo kupelekea kutokuwa na imani na katibu huyo kwani mara
nyingi wamekuwa wanaitaji kujua mwenendo mzima wa fedha zilizotumika kujengea
moja ya darasa la shule hiyo.
Hata hivyo viongozi
hao wameongeza kuwa katibu huyo amekuwa ataki kusikiliza ushauli wa mwenyekiti
wake na hivo kupelekea kutokuwa na sitofahamu baina yake yeye na mwenyekiti
wake ambao wanaosimamia kamati hiyo ya
ujenzi na hivo kupelekea wananchi kutopata takwimu ya mapato na matumizi kwa
mwaka uliopita.
Best fm ilifanikiwa
kumtafuta katibu huyo kwa njia ya simu
juu ya kubainisha swala ilo ambapo kwa upande wake amefafanua kuwa mara nyingi amekuwa anamwomba mwenyekiti
wake ili awafahamishe wananchi wake juu ya mapato na matumizi ya mwaka jana
ambapo mwenyekiti huyo amekuwa anatingwa na shughuli za kilimo
Ludewa yetu na maendeleo yetu
No comments:
Post a Comment