“Wana mategemeo au walikuwa nayo juu yangu na nimeshindwa kuyatimiza. Hivyo najisikia vibaya kwa sababu hiyo.”
Wakati huo huo jana timu ilishindwa kufanya mazoezi kama ilivyo utaratibu wao kufanya mazoezi ya kupasha misuli siku moja baada ya mechi.
Boss huyo wa zamani wa United alisema klabu inataka timu icheze soka la kuvutia – na Van Gaal, ambaye alisafiri kwenda Holland jana, ameshindwa kufanikisha hilo.
Gill alisema: “Bila shaka msimu huu umekuwa sio wenye mafanikio ukiangalia na uwekezaji uliofanyika katika usajili.”
Van Gaal, 64, ametumiwa kiasi cha £250million tangu aliporithi mikoba ya Moyes miezi 18 iliyopita lakini klabu imekuwa kifanya vibaya.
Gill aliongeza: “Siwezi kukaa hapa na kuongopa kwamba soka linavutia – kwangu mimi, tulichokifanya zamani kilikuwa kizuri. Tunataka soka la kuvutia.”
Ludewa yetu na maendeleo yetu
No comments:
Post a Comment