Thursday, October 22, 2015

RONALDO AONYESHA MAPENZI MAKUBWA KWA SHABIKI ALIYEVAMIA

Cristiano Ronaldo ameonyesha mapenzi ya juu kwa shabiki aliyevamia uwanjani.

Shabiki huyo alivamia uwanjani wakati Madrid ikipambana na PSG iliyokuwa nyumbani jijini Paris, Ufaransa.
Ilikuwa ni mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, shabiki huyo alikatiza kwa kasi ya kimondo. Alipomfikia Ronaldo, alimpokea na kumkumbatia.
 
Hata wakati walinzi wa uwanja wanaingia, Ronaldo aliwazuia kumpa kipigo, akapiga naye stori sekunde kadhaa na kuwaruhusu wamchukue lakini si kwa kumpiga.
Baada ya hapo mashabiki walimshangilia kwa kile alichoonyesha kwa shabiki huyo aliyeonyesha mapenzi makubwa kwake.

Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko

No comments:

Post a Comment